Sunday , 2nd Jul , 2023

Muungano wa Azimio la Umoja chini ya Raila Odinga umedai utamuondoa mamlakani Rais William Ruto na serikali yake. Viongozi hao wa Azimio wametoa angalizo dhidi ya serikali ya Kenya wakidai kuwa wameshindwa kukidhi mahitaji ya mwananchi wa kawaida.

Mbunge wa Saboti, Caleb Amisi amesema kuwa ni rahisi sana kumuondoa Ruto madarakani kwa sababu alishinda kwa kura chache katika uchaguzi

Kwa upande wa Kiongozi wa Azimio Raila Odinga amewataka wananchi kuwa na angalizo na serikali ya Kenya Kwanza huku akisema muswada wa fedha 2023 utakuwa na athari kubwa kwa wananchi na hivyo wanafaa kuukataa mara moja kwa kususia kulipa ushuru.

“Tuliwaambia punda amechoka Hawakutuskiza. Wamezidi kuwekelea mizigo punda mgongoni. Sasa wakati umefika punda sasa awapige mateke"-Amesema  Raila.