Wananchi waliobeba mwili wa mfanyabiashara
Mke mdogo wa marehemu huyo,Mwanaidi Isah, amesema kwamba mume wake usiku wa kuamkia jana alilala kwa mke wake mkubwa na aliporudi kwake alikuwa akilalamika kuwa tumbo linamuuma na baada ya hapo alimuagiza dukani akachukue sabuni lakini aliporudi alikuta mume wake huyo tayari kashajinyonga.
"Mume wangu alilala kule Donge kwa mke mwenzangu alfajiri alikuja kwangu hapa Makorora akilalamika kuwa tumbo linamuuma akanituma nikamletee sabuni dukani kwetu niliporejea nikamkuta stoo akiwa ameshajinyonga" amesema Mwanaidi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe amesema bado wanachunguza chanzo kilichopelekea mfanyabiashara huyo kujinyonga.