Wednesday , 7th Jun , 2023

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), imewataka Watanzania kupuuza taarifa za upotoshaji zinazofanywa kwa makusudi na watu wenye nia ovu zinazodai serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Dubai kandarasi ya uendeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka 100.

Bandari ya Dar es Salaam

TPA imefafanua azimio la Bunge linahusu mkataba ambao serikali inaingia na serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi 12 kwa ajili ya kutoa nafasi kujadiliana kuhusu maeneo ambayo nchi hizo zinaweza kushirikiana katika uboreshaji na uendelezaji wa sekta ya bandari nchini Tanzania.

Ushirikiano wa nchi hizo mbili una lengo la kuongeza ufanisi wa huduma za bandari nchini, kukuza ajira za Watanzania na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji kwenye baadhi ya maeneo ya bandari ya Dar es Salaam, maeneo huru ya kiuchumi na viwanda.