Friday , 2nd Jun , 2023

Festo Lusasi mkazi wa Mwangata mkoani Iringa, ameiomba serikali na jamii kumsaidia huduma za matibabu baada ya kupata ajali ya gari mwaka 1994 na kusababisha mwili wae kupooza kuanzia kiunoni hadi mguuni.

Festo Lusasi

Kutoa ni moyo na si utajiri kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia anaweza kuwasiliana naye kupitia namba ya simu 0754 206 287.

"Nilipata ajali ya gari nilikuwa naenda vijijini kufika njiani gari ikapata tatizobikaanguka, toka nilipopata ajali nilikuwa na mke, baada ya kukaa muda mrefu akaamua kurudi nyumbani kwao, naishi kwa ndugu yangu ananisaidia," amesema Festo 

Festo anasema ajali hii ilikatisha ndoto za maisha yake na kulazimika kuishi kwa shemeji yake ambaye anamuuguza hadi sasa

Mama mzazi pamoja na ndugu zake Festo, wameeleza kuwa hali ya kiuchumi wanayopitia ni ngumu na kuwaomba wasamalia wema kuwasaidia.