Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

BBT Mifugo kuwezesha vijana nchini

Thursday , 1st Jun , 2023

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kufuatia Mkoa wa Tabora kuongoza kwa  kuwa na idadi kubwa ya mifugo hapa nchini wamepanga kuanzisha programu kabambe ya BBT Mifugo itakayowawezesha vijana kunenepesha mifugo na  kuufanya mkoa huo kuwa kinara na lango kuu la kuuza nyama

Waziri Ulega aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara aliyoufanya Wilayani Kaliua mkoani Tabora 
Amesema Tabora ni mkoa uliobarikiwa kuwa na eneo kubwa la ardhi na rasilimali nyingi ya mifugo hivyo anaona mkoa huo una kila sababu ya kuwa kinara wa kufanya biashara ya mifugo.

"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, tunataka kuufanya mkoa wa Tabora kuwa ndio lango la kuvunia mifugo, vijana wawekeze kwenye mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa mifugo na mazao yake ili waweze kuuza nyama  ndani na nje ya nchi, na wakiweza kufanya hivyo watakuza kipato chao na Taifa kwa ujumla", alisema

"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, sisi tupo tayari kuanzisha programu ya BBT hapa Tabora  kwa sababu rasilimali ipo ya kutosha hivyo ni rahisi kupata matokeo kwa haraka, muhimu ni kuifungamanisha rasilimali hiyo katika mnyororo wa thamani kuanzia uzalishaji mpaka katika masoko", alifafanua

Alisema kwa kuwa programu hiyo walishaianzisha katika Mikoa ya Mwanza, Kagera na Tanga hivyo ni rahisi kuanzisha pia mkoani Tabora, na mipango ni kuifanya BBT Mifugo ya Tabora kuwa ya kwanza katika ufugaji bora na uuzaji wa nyama.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi. Dkt. Batilda Burian alimshukuru Waziri Ulega kwa mipango hiyo, huku akimuhakikishia kuwa tayari wana eneo la hekari 6000 lililopo Wilayani Kaliua  ambalo watalitumia kwa ajili ya programu hiyo ya BBT Mifugo. 

Aidha, alisema pia kuna hekari nyingine 40,000 ambazo zipo Wilayani  Nzega ambazo watazitumia pia kufanya ufugaji wa kisasa ikiwemo kulima malisho kwa ajili ya mifugo yao na kuuza ndani na nje ya nchi.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani