
Naibu Mkuu wa Takukuru Kagera, Ezekiel Senkala
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu, naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera, Ezekia Senkala amesema kuwa uchunguzi uliofanyika katika kipindi hicho pia umebaini uwepo wa wafanyabiashara wanaofanya biashara ya mifugo bila leseni.
"Hatua zilizochukuliwa katika kudhibiti upotevu huu wa fedha, ni kuzitaka halmashauri kuanza kutumia watendaji wa vijiji pamoja na maafisa ugani kuongeza nguvu siku za minada, ili kudhibiti ukwepaji wa ushuru, lakini pia kuwabaini wafanyabiashara wa mifugo wasio na leseni, ili wakatiwe leseni na kufanya biashara kwa mujibu wa taratibu" amesema Senkala.
Nao baadhi ya Wananchi waliozungumza na EATV kuhusiana na baadhi ya watumishi kushindwa kukusanya ipasavyo mapato ya serikali, wameshauri wananchi kuendelea kufundishwa uzalendo