Tuesday , 17th Feb , 2015

Star wa muziki wa Injili wa nchini Kenya, Ringtone ameamua kuingia mitaani kukutana na watoto wasio na makazi maarufu kama machokoraa.

Ringtone

Ringtone ameamua kufanya haya ikiwa ni mkakati wake wa kutoa msaada na elimu yenye lengo la kuwabadilisha na kuwatoa katika mtindo wa maisha wanayoishi.

Ringtone ambaye binafsi amekuwa ni moja kati ya watu waliokulia katika maisha magumu ya namna hiyo na kuweza kubadilika na kujipatia mafanikio, ameamua kutumia nafasi na uwezo alionao kujaribu kusaidia watoto hao, akiwa na imani kuwa na wao wana nafasi ya kubadilika.

Hatua ya Ringtone inakuja kama moja ya jitihada zake nyingi za kurejesha kwa jamii shukrani kutokana na nafasi yake kama moja ya wasanii wa muziki wenye mafanikio makubwa nchini Kenya.