
Tuzo hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule kwa niaba ya wanajukwaa wakati wa kongamano kubwa la Wajasiriamali wakina mama wa mkoa wa Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa kanisa katoliki la Mt Paulo Msalaba.
Akitoa maelezo ya awali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wajasiriamali wanawake mkoa wa Dodoma Bi.Maryrobbi Mabhaya amesema tuzo hiyo imetolewa maalum kwa ajili ya kuthamini na kuenzi mchango mkubwa wa Mbunge Mavunde kwa maendeleo ya wakina mama Dodoma na hasa katika kuwatafutia fursa na uwezeshwaji kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.Rosemary Senyamule amempongeza Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo amekuwa karibu na wakinamama katika eneo la uwezeshwaji kiuchumi na akatumia fursa hiyo kuwataka wakina Mama wa Dodoma kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hasa katika eneo la kilimo cha mashamba makubwa ya pamoja(block farms).
Aidha,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh.Anthony Mavunde amewashukuru wakina mama wa Dodoma kwa kutambua mchango wake katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi ya wakina mama Dodoma na kuahidi kuja na programu mbalimbali nyingi zaidi za kuwajengea uwezo na kuwawezesha wakina mama ikiwemo hatua ya sasa ya kutafuta Taasisi ya fedha ambayo itawakopesha wakina mama wajane bila riba.