Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ugonjwa usiojulikana Bukoba ni 'Marburg'

Tuesday , 21st Mar , 2023

Serikali imetangaza mpaka sasa ugonjwa  ulioripotiwa Machi 16, 2023 kutoka Wilayani Bukoba, umejulikana kuwa ni virusi vya 'Marburg'' na hadi wakati huu tayari umekwishaua watu watano huku walioathirika wakiw ni 8 na watatu kati ya hao wanaendelea na matibabu.

Akizungumza na Wanahabari, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kwamba ugonjwa huu ambao kwa mara ya kwanza uligundulika huko Mji wa Marburg chini Ujerumani.

Akizungumzia kuhusu uambukizaji wa ugoonjwa huo, Waziri amesema "Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine ambapo, kama utashika maji maji pale ambapo pana uwazi au mtu ana michubuko ama kidonda, na maji maji hayo yanaweza kuwa Damu, mate, mkojo, machozi yatokayo kwa maiti ama kwa mgonjwa mwenye dalilili ya ugonjwa huo"  

Mpaka sasa Serikali imedhibiti ugonjwa huo kusambaa kutoka nje ya wilaya, na kwamba tangu wagonjwa huo waliporipotiwa Bukoba mpaka sasa haujavuka kwenda sehemu nyingine.

Aidha ameeleza kwamba baadhi ya dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kuumwa kichwa, kuharisha, kuishiwa nguvu, kutoka damu sehemu za mwili zilizo wazi.

Mbali na hayo, Waziri Ummy ameweka wazi kuwa Ugonjwa huo hauna tiba mahsusi isipokuwa mtu atatibiwa kutokana na dalili atakazo kuwa nazo.

Hata hivyo Waziri huyo amesisitiza Ugonjwa huo sio tishio kwa kuwa unaweza kudhibitika  na kwamba mpaka sasa serikali inawatazama kwa makini watu 161 ambao kwa namna moja ama nyingine walipata kushirikiana moja kwa moja na waathirika wa ugonjwa wa Marburg.

Aidha Shirika la Afya duniani (WHO) imeeleza kwamba ugonjwa huu si mara ya kwanza kutokea Afrika na kwamba miaka kadhaa nyuma umeshawahi kutokea katika nchi jirani ya Uganda.

HABARI ZAIDI

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu