Saturday , 17th Dec , 2022

Shirika la Reli Tanzania TRC limesema litaona uwezekano wa kuongeza safari zake kutoka mbili hadi nne kwa wiki kutoka mkoani Kigoma hadi Dar Es Salaam, kufuatia serikali kuongeza mabehewa mapya ambayo yamepokelewa na viongozi na wananchi Mkoani kigoma

Baadhi ya wananchi wakizungumza mara baada ya mabehewa hayo kuwasili mjini Kigoma, wamepongeza serikali na kwamba kuongezwa siku za safari kutaongeza kasi ya mzunguko Kibiashara

Kwa upande wake Mbunge anayewakilisha kundi la Wanawake Mheshimiwa Zainabu Katimba na Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini Mheshimiwa Kirumbe Nge’enda wamesema mabehewa hayo yatawaondolea wananchi msongamano wa kusubiri safari za treni na kuongeza tija katika masuala ya kiuchumi

Aidha Mkurugenzi wa uendeshaji shirika la Reli Nchini TRC Focus Makoye amebainisha kuwa hakuna mabadiliko ya bei sa safari kutokana na kuanza safari za mabehewa hayo mapya na kuwataka wananchi kuzingatia usafi na kutunza miundombinu hiyo.