Saturday , 7th Feb , 2015

Katika jitihada za kuongeza ladha na ujuzi zaidi katika kazi yao ya muziki, Kundi mahiri la Makomandoo wametangaza rasmi kuongeza nguvu kazi katika kikosi chao.

Kikosi kipya cha mashambulizi cha Makomandoo

Wakali hao kwa sasa wanakamilisha idadi ya watu 5 wenye uwezo wa kulishambulia jukwaa na kutoa burudani iliyojitosheleza.

Wakali wa kundi hili, Muki pamoja na Fredwayne wamesema kuwa, wasanii hawa wapya ambao wanaongeza nguvu kwa upande wa kudansi katika kundi hili ni usajili mpya ambao ndani yake kuna Sheddy pamoja na Rai, wakali ambao pia wameweza kuonekana katika show ya FNL wakionesha uwezo wao usiku wa jana.