Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

CITI Bank kushirikiana na serikali ya Tanzania

Wednesday , 23rd Nov , 2022

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwingulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka CITI Bank Unaosimamia Ukanda wa  Jangwa la Sahara na Mashariki ya Kati

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (wa nne kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Citibank, Bw. David Livingstone (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Ujumbe kutoka Citibank baada ya kumalizika kwa kikao chao jijini Dar es Salaam.

Benki hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika uendelezaji wa miradi ya maendeleo, uwekezaji na kufanya tathimini ya  uwezo wa`nchi kukopesheka (credit rating).

Dkt. Nchemba amefanya kikao jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa CITI group Bw. David McD. Livingstone amesema Benki yake inajivunia kufanyakazi na Tanzania katika kufikia agenda yake ya kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Dkt. Nchemba. alielezea kuwa wamejadiliana namna ya kuharakisha ukamilishaji wa suala la tathimini ya uwezo wan chi kukopesheka katika masoko ya kimataifa (credit rating) ndani ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo CITI Group ndio  washauri wakuu wa zoezi hilo. 

Alisema kuwa Serikali inaendelea kujadili na kuhakikisha kuwa utekelezaji wa miradi mingine ambayo wao wanahusika moja kwa moja kama vile mradi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na miradi mingine ya maendeleo ambayo serikali iliwahusisha katika utafutaji wa fedha ili kukamilisha miradi iliyopo kwenye mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Dkt. Nchemba alisema kuwa jambo la kuendeleza ushirikiano katika masuala ya kitaalamu hasa hilo la creding rating pamoja na masuala ya uhamasishaji wa upatikanaji wa rasilimali fedha ambazo Serikali inazipata  kutoka Taasisi mbalimbali za fedha  Benki kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR) pamoja na miradi mingine ya maendeleo.

“Tumekubaliana pia katika mazungumzo yetu kwamba wasimamie wito uliotolewa na Mhe. Rais ya kuwaalika wawekezaji kama vile taasisi za kifedha na sekta binafsi kwa kuwa wana mtandao mkubwa katika maeneo tofauti tofauti ili  waje wawekeze na kutumia fursa zilizopo nchini hususan utengenezaji bidhaa ambazo zimepanda bei kama mafuta ya kula, mbolea pamoja na unga wa ngano” alisema Dkt. Nchemba

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa CITI group Bw. David McD. Livingstone amekukubali kuendelea kushirikiana na serikali kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo na pia kukamilisha zoezi la kutathimini na  kuangalia uwezo wa nchi kuweza kukopa na kulipa madeni na kuhahakikisha kwamba zoezi hilo linakamlika ndani ya muda uliopangwa na kuhamasisha uwekezaji kutoka Sekta Binafsi ili waweze kuchangia maendeleo ya nchi.
 

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani