
Mkurugenzi huyo ametoa taarifa hiyo akiwataka wananchi kuendelea na utulivu mpaka uchunguzi utakapo kamilika akibainisha kuwa kila tukio linapotokea linaacha somo kwa wadau katika sekta akiwataka watu kuendelea kupata taarifa sahihi kutoka vyanzo sahihi.
Kuhusu suala la fidia kwa wahanga amesema shirika liko na bima na tayari taratibu za mawasiliano na wahanaga zinaendelea kuwajuza nini kinatakiwa ilikupata stahiki zao ikihusisha jumuiya ya kimataifa na inafanyika kwa faragha baina ya muhanga na kampuni
Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuwashukuru watanzania serikali kuanzia kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna walivyolipokea na kulishughulikia suala la ajali Na watahakikisha kila kitu kinaenda kwa utaratibu.