Wednesday , 26th Oct , 2022

Mkoa wa Dar es Salaam umetekeleza Agizo la Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu afua 14 za lishe alilotaka Kila manispaa kutumia mapato yake ya ndani kuhakikisha inatenga bajeti kutokomeza udumavu na utapiamlo Kwa watoto.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla.

Mapema hii Leo zoezi la utiaji Saini wa afua 14 za lishe limesainiwa na wakuu wa wilaya za mkoa wa Dar es Salaam mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Kwa ajili ya utekelezaji wa upatikanaji wa chakula mashuleni ambapo Mhe Rais aliagiza Kila mtoto chini ya Miaka mitano atengewe Shilingi elfu Moja Kwenye bajeti huku mkuu wa Mkoa huo Amos Makala  akiwataka wakuu wa wilaya zote za Dar es Salaam kuwa na mikakati ya utekelezaji.

Kwa mwaka  wa 2021-2022 takwimu zilionesha mkoa wa Dar es Salaam kuongoza katika utekelezaji wa mikataba iliyosainia sambamba utoaji wa chakula huku manispaa ya Temeke Kwa Dar es Salaam ikitekeleza Kwa ufanisi afua 12 kati ya 14 zilizosainiwa.

Pia wito umetolewa Kwa wazazi na walezi pale inapobidi kuungana na kamati za shule kuchangia sehemu Ili kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni hali inayotajwa kuongeza ufaulu Kwa wanafunzi.