
Harriet Lwakatare, Mkurugenzi huduma kwa wateja Vodacom Tanzania
Harriet Lwakatare ambaye ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania, amesema Kila mwaka huwa wanasherekea wiki ya huduma kwa wateja, lakini kwa mwaka huu wanafanya hivyo chini ya kaulimbiu ya ‘tunasherekea kukuhudumia’ .
Kwa upande wake mmoja kati ya wateja wa Vodacom ambaye ni mlemavu wa miguu, Bw. Ernest Justin ameeleza namna dawati hilo maalum lilivyo mhimu kwao, na kwamba kama mtu mwenye ulemavu amefurahi sana kuona wamepewa kipaumbele na Vodacom, huku akisema kuwa walichokifanya ni zaidi ya upendo na kuyaomba makampuni mwengine nchini kuiga kilichofanywa na Vodacom.
“kwakweli sisi hasa mimi mwenyewe kama mtu mwenye ulemavu nimefurahi sana kuona tumepewa kipaumbele na Vodacom, hiki walichokifanya ni zaidi ya upendo kwetu kwamba sasa kama mtu ni kipofu au kiziwa atahudumiwa na watu wajuzi wa lugha za alama. Na pia niyaombe makampuni mwengine nchini kuiga kilichofanywa na Vodacom. Wametuthamini sana kwa kuanzisha dawati la watu wenye mahitaji maalum" - Ernest Justin - Mteja wa Vodacom.