Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kiduku, Mandonga waisimamisha Mtwara

Wednesday , 21st Sep , 2022

Mabondia Twaha Kiduku na Karim Mandonga jana asubuhi alisimamisha shughuli za kiuchumi kwa muda kutokana na kupewa mapokezi mazito chini ya mkuu wa mkoa, Kanali Ahmed Abasi Ahmed kuelekea kwenye pambano la kimataifa la Mtwara Ubabe Ubabe 2 linalotarajia kupigwa Septemba 24, mwaka huu.

Katika mapokezi hayo ambayo yaliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dustan Kyobya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkoa kutokea katika uwanja wa ndege wa Mtwara kwa kuzunguka mitaa mbalimbali ya mkoani hapa kabla ya kwenda kwa mkuu wa mkoa, Kanali Ahmed Abasi Ahmed ambaye aliwakaribisha mabondia hao mkoani hapa.

 Kanali Ahmed alisema kuwa anawakaribisha mabondia hao mashuhuri nchini ndani ya mkoa huo pamoja na kuwatakia ushindi katika pambano lao l la Mtwara Ubabe Ubabe 2 huku akitoa wito kwa wadau kujitokeza kuweza kwenye mkoa huo kupitia sekta ya utalii kutokana na vivutio walivyokuwa navyo.

“Nadhani nisiwe mzungumzaji sana lakini kubwa nawakaribisha Mtwara pamoja na kuwatakia ushindi katika pambano la Mtwara Ubabe Ubabe 2, nichukue tena fursa hii kuwaomba wadau na kuwapongeza wote walioshiriki katika jambo hili kwa kuutangaza mkoa wa Mtwara na huu ndiyo wakati wa wawekezaji kuja kuweza kwenye mambo mbalimbali yakiwemo ya utalii kwa sababu tuna vivutio vingi hapa,” alisema  Kanali Ahmed. 

Kwa upande wa Kiduku na Mandonga  wameshukuru kwa mapokezi  hayo makubwa pamoja na kamati  yote ya maandalizi ambapo kila mmoja ameahidi kutoa zawadi  ya ushindi siku ya Jumamosi kwa kuhakikisha anashinda pambano lake.

 Ikumbukwe Kiduku atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa UBO dhidi ya Abdo Khaled kutoka Misri wakati Karim Mandonga akitarajia kupanda ulingoni dhidi ya Salim Abeid kutoka Tanga.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani