Mkurugenzi wa TAKUKURU Hamduni Masauni
Akizungumza wakati wa kutamatisha mafunzo hayo Mkurugenzi wa kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Hamduni Masauni amesema suala la ukaguzi ni suala endelevu na wamefanikiwa kukuta waajiriwa wapya 6 vyeti vyao vikiwa na utata na waajiriwa wapya 2 wakikutwa na vyeti vya kufoji
Naibu waziri wa nchi ofisi ya raisi Management na utumishi wa umma na utawala Bora Deogratius Ndejembi amesema hatarajii kuona wahitimu hao wakiwa wamelewa baada ya kuhitimu mafunzo hayo badala yake wakawe mabalozi katika jamii ambazo watakwenda kuishi.
Nae mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdini Babu amewataka wahitimu hao wanapokwenda katika vituo vya kazi wafanye kazi kwa ueledi, hekima na busara katika kufanya kazi kwani zipo changamoto mbali mbali katika jamii na wao ndio wakuzitatua