Friday , 9th Sep , 2022

Watoto wa mfalme Zumaridi hii leo Septemba 9, 2022, wamefika mahakamani kufuatilia kesi ya mama yao, watoto hao pia waliongozana na Bibi yao.

Mfalme Zumaridi akiwa na watoto wake mahakamani

Zumaridi na wafuasi wake nane wanakabiliwa na kesi ya kujeruhiwa askari polisi na kuwazuia kutekeleza majukumu yao inaendelea na ushahidi, huku kesi ya usafirishaji haramu wa binadamu inayomkabili yeye mwenyewe ikitarajiwa kutajwa tena.

Kesi hiyo nambari 10 ya mwaka 2022, ya kuwazuia askari majukumu yao inaendelea na ushahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza.