Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa
Sri Lanka imekua kwenye mdororo mkubwa wa uchumi huku umati wa watu waliovamia Ikulu kuanza kutapanya mali za za ofisi hiyo kuu ya nchi, ikiwemo kuogelea kwenye bwawa la Ikulu na kuichoma moto nyumba ya Waziri Mkuu wakisema kwamba hawataondoka mpaka Rais huyo ang'atuke kabisa .
Hapo awali Spika wa Bunge la nchi hiyo alisema kuwa Rais angejiuzulu keshokutwa yaani Julai 13 mwaka huu.
Rais Rajapaksa, ambaye hajulikani alipo hajaongea lolote hadharani toka makazi yake yavamiwe Jumamosi iliyopita.
Vyanzo vya habari vinasema kuwa alitoroshwa kukimbizwa eneo salama kupitia njia ya maji kabla waandamanaji hao hawajavamia Ikulu.