Aurelian Tchouameni
Madrid wamekamilisha usajili huu kwa ada ya uhamisho ya Pauni millioni 85 sawa na Bilioni 244,564,785,020.98 kwa pesa za Tanzania na amesaini mkataba wa miaka 6 utakaomalizika Juni 2028. Kiungo huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 atafanya vipimo vya afya Jumanne wiki ijayo Juni 14, 2022 na kutambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari na mashabiki.
Real Madrid wamethibitisha usajili wa Tchouameni kupitia mtandao wao wa kijamii wa Tweeter ambapo waliposti picha ya mchezaji huyo na kuandika karibu Tchouameni. Klabu za Liverpool ya England na PSG ya Ufaransa nazo zilikuwa zimeonyesha nia yakutaka kumsajili kiungo huyu.
Msimu uliopita Aurelian Tchouameni alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha AS Monaco ambapo alicheza michezo 50 kwenye michuano yote na alifunga mabao 5 akiisaida Monaco kumaliza nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu nchi Ufaransa msimu uliopita wa 2021-22.

