Wednesday , 21st Jan , 2015

Wakuu  wa  nchi  za  Tanzania,  Kenya na  Uganda  wamekutana  jijini  Arusha  na  viongozi  wa  nchi  za  Sudan  na  Sudani  Kusini zinazokabiliwa  na  mapigano   ikiwa  ni sehemu  ya  jitihada  za  kutafuta  suluhu  ya  mgogoro  huo.

 
Lengo  la  kukutana  kwa viongozi  hao  ni  kushuhudia  utiaji  saini  wa  makubaliano  ya  mazungumzo  yaliyokuwa  yanaendelea  kwa   usimamizi  na  uratibu  wa  chama cha  mapinduzi  chini  ya  uenyekiti  wa makamu  mwenyekiti  mstaafu  wa  CCM  mzee John  Malechele.

Baada   ya  mazungumzao hayo  kuanza  mwezi  Oktoba  mwaka  jana   viongozi  wa chama  tawala  cha  (SPLM)  ambacho  kimegawanyika  makundi  matatu  moja  likiwa  kundi  lililoko  madarakani  chini  ya   Rais  Salva  Kiir.

Kundi la pili linaloongozwa  na aliyekuwa makamu wa  Rais    Dkt  Rieck  Machar  na la Tatu  ni  lile  la waliokuwa wafungwa wa kisiasa  wamekutana mara  kadhaa  jiji  Arusha   ambapo  walikubaliana  kusaini  mkataba wa kumaliza  mgogoro   huo,   zoezi  ambalo    hadi  muda  huu   halijafanyika  na  mazungumzo  yanaendelea.

Viongozi  waliiwasili  jijini   Arusha  kwa  lengo la kushuhudia  utiaji  sahihi  huo  ni    pamoja  marais   Dkt  Jakaya  Kikwete  wa  Tanzania, Uhuru  Kenyata  wa  Kenya  na Yoweri Museven  wa Uganda.

Wengine  ni pamoja  na  Makamu  wa  Rais  Tanzania  Dkt  Mohamed   Gharibu Bilal , Makamu wa Rais  wa Afrika Kusini   Sirili  Ramafosa,  na   mawaziri  na watendaji  wa  sekta mbalimbali.