
Mwenyekiti wa soko hilo Daniel Ibrahim amethibisha uwepo wa wafanyabiashara wengi waliokuwa na mikopo na sasa hawajui nini cha kufanya wakiomba serikali kuwatazama upya.
Kufuatia sintofahamu hiyo tumemtafuta Mwanasheria Khamis Masaoud kuzungumzia endapo mtu amekopa na yakatokea majanga ipi ni nafuu yake kisheria licha ya kwamba tayari upande mmoja wa mkataba ulikuwa ukitekeleza majukumu yake kabla ya janga Kutokea.
Utakumbuka ni majuzi tu maswali kama haya yaliwakuta wafanyabiashara wa soko la Kariakoo, mbagala,Karume na soko la Ilala noma Mara baada kupoteza biashara zao Kwa kuunguliwa na moto.