Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa Kodi kutoka TRA
Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 22, 2022, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, na kusema kwamba mkutano wa awali walioketi hapo jana na wataalam hao ulikuwa ni wa wao kuelewa mazingira ya sheria ya kodi pamoja na wao kueleza jinsi wanavyotozwa kodi kwenye nchi zingine.
"Lengo ni kufikia mahali huko mebeleni kampuni hiyo iweze kuchangia kodi kutokana na biashara inayofanyika hapa nchini kupitia mitandao yao, wananchi wasiwe na hofu," amesema Richard Kayombo