Thursday , 21st Apr , 2022

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde amewaagiza viongozi wa ushirika wa zabibu UWAZAMAM kuhakikisha unawalipa wakulima haraka malipo ya zabibu zao walizonunua. 

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde

Naibu Waziri Mavunde ametoa maagizo hayo leo April 21/2022 alipofanya kikao cha pamoja na wakulima wa zabibu, Uongozi wa UWAZAMAM pamoja na benki ya TADB.

"Haiwezekani wakulima walete zabibu zao kwenu, ambazo mmezichakata na kuwa mvinyo gafi, wamekaa zaidi ya mwezi wakisubiri malipo yao zaidi ya milioni 200, ni lazima viongozi muwajibike kutafuta suluhu ya haraka na kuwalipa wakulima.

Mavunde amesema Serikali inatamani kuuona ushirika huo wa wakulima wa Zabibu unakua na kujenga kiwanda chake wenyewe cha uchakataji wa zabibu, hivyo lazima waanze sasa kuweka misingi bora na kuwasaidia kufikia malengo yao