Saturday , 9th Apr , 2022

Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe, ameilaumu bodi ya pembejeo inayosimamia ununuzi wa salfa na viuatilifu vingine vya Korosho kwa kutotenda haki kwa baadhi ya wazabuni huku akimshauri Waziri wa Kilimo kumthibitisha Mkurugenzi Bodi ya Korosho au kumuondoa kwa kuwa amekaimu muda mrefu.

Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe

Mh. Mwambe ameyasema hayo katika kikao cha wadau wa korosho kilichofanyika katika ukumbi wa PSSF jijini Dodoma, kilichoandaliwa na bodi ya korosho kikao kilichokua chini ya uenyekiti wa Waziri wa Kilimo, kikihudhuriwa pia na Wabunge, na Wakuu wa Mikoa inayolima Korosho ya Tanga, Pwani,  Ruvuma, Lindi na Mtwara.

Aidha Mh. Mwambe amebainisha kuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) amekuwa akitumia fedha ya bondi inayowekwa na wanunuzi kuiweka fixed deposit, hivyo akataka kufahamu matumizi na faida inayopatikana sambamba na matumizi ya 5% zinazokatwa kwa ucheleweshwaji.