(Nyota wa Los Angeles Lakers, Lebron James)
Lebron amefikisha alama hizo baada ya kufunga alama 36 kwenye mchezo wa alfajiri ya kuamkia Jumapili ya Machi 20, 2022 dhidi ya Washington Wizard ambapo Lakers walifungwa kwa alama 127-119 na kusalia kwenye nafasi ya 9.
Lebron amempiku gwiji wa zamani wa NBA, Karl Malone anayeshika nafasi ya tatu mwenye alama 36,928 huku kinara wa ufungaji mwenye alama nyingi zaidi kwenye historia ya NBA ni Gwiji Karim Abdul Jabar mwenye alama 38,387.
Baada ya Lebron kuweka rekodi hiyo, baadhi ya wapenzi na wafuasi wa mchezo huo Ulimwenguni wameibua mjadala wakidai kuwa, Lebron ndiyo mchezaji bora wa NBA katika kipindi cha miaka 15 iliyopita mbele ya Kobe Bryant.
Kwenye orodha hiyo ya wafungaji alama nyingi, magwiji wa zamani wa NBA Kobe Bryant anashika nafasi ya nne akiwa na alama 33,643 huku Michael Jordan akishika nafasi ya tano akiwa na alama 32,292.