
Picha ya H Baba kulia kushoto ni Zuchu
Kupitia Instagram yake H Baba amepost picha ya Zuchu na kushusha maneno yafuatayo "Kama nitakubaliwa nikipata bahati hii nitakuwa tayari kumuoa @officialzuchu kama mtaniondolea vikwazo nimejipanga nipo tayari niambieni niandae Ng'ombe wangapi au nifanyeje".
"Zuchu ni muislam mwenzangu lolote linaweza tokea, acha niandae wazee wangu wakisukuma wakamuone mama pia baba yake kule Zenji, ningependa nimuoe ni binti mstaarabu sana, acha nifate taratibu za kidini".