Monday , 22nd Dec , 2014

Msanii wa muziki Phina Mugerwa, amekuwa na kipindi kizuri cha mwisho ya mwaka kutokana na tukio la kuvunjika kwa penzi la Baba wa Mtoto wake, Ken Muyiisa na msanii wa muziki Cindy Sanyu.

Msanii wa Muziki wa nchini Uganda Phina Mugerwa akiwa na mtoto wake

Phina tayari amekwishaanza kushiriki furaha yake hii na mashabiki wake mitandaoni kwa kuweka picha za Ken akiwa na mtoto wao kuonesha kuwa baba amerudi nyumbani, na vilevile kuthibitisha usemi wake kuwa hakuna mwanamke anayeweza kumuibia mwanaume wake.

Mpaka sasa hakuna tamko rasmi kutoka kwa Cindy wala Ken kuhusiana na kutengana kwao, ikikumbukwa kuwa wawili hawa walikwishafikia mpaka hatua ya kwenda kutambulishana kwa wazazi, wakiwa na matarajio makubwa ya kufunga ndoa baadaye.