James Nandwa
Kocha huyo anachukua mikoba iliyoachwa na Kocha Yusuph Chippo aliyekwenda nchini kwao Kenya kutokana na matatizo ya kifamilia kuwa kwenye hali ambayo sio mzuri jambo ambalo lilipelekea kushindwa kurejea nchini kwa ajili ya kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Akizungumza mara baada ya kutua jijini Tanga leo ikiwemo kulakiwa na viongozi wa klabu hivyo wakiongozwa na Meneja wake ,Akida Machai wakiwemo Katibu Mkuu pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji,Kocha huyo alisema kuwa dhamira yake kubwa ni kuhakikisha anaipa mafanikio timu hiyo.
Akizungumza leo, Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa ujio wa kocha huyo utawezesha timu hiyo kufikia malengo yao ambayo wamejiwekea ya kuhakikisha wanachukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Assenga amesema kuwa kutokana na uzoefu aliokuwa nao kocha huyo utawezesha kupelekea chachu kwa wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho kupambana wakiwa na lengo la kuipa mafanikio timu hiyo.
Kwa upande wake,Kocha Nandwa amesema kuwa kitu cha kwanza ni kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yake iliyojiwekea ya kuwa timu bora Tanzania ili iweze kupata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya kombe la shirikisho.
“Kwanza nashukuru kupata nafasi ya kuifundisha Coastal Union nitahakikisha nitaifikisha timu hii kwenye malengo waliojiwekea ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara kutokana na uzoefu wangu niliokuwa nao “Amesema Nandwa.
Kocha Nandwa aliwahi kuzifundisha timu za soka za Harambee Stars, AFC Leopard ya Kenya pamoja na Utalii ya Kenya na kuipa mafanikio makubwa ikiwemo Ubingwa wa Ligi kuu nchini humo.