Saturday , 14th Aug , 2021

Klabu ya Real Madrid ya Hispania imekanusha taarifa zinazoripotiwa kuwa timu hiyo inampango wakujitoa kushiriki Ligi Kuu ya Hispania La Liga na kujiunga na Ligi Kuu ya England EPL, kutokana na migogoro baina ya klabu hiyo na Rais wa La Liga Javier Tebas.

Rais wa Real Madrid Florentino Perez

Kwa mujibu wa taarifa  iliyoripotiwa na gazeti la Mundo Deportivo iliripoti kuwa Rais wa Real Madrid Florentino Perez ameanza mipango yakuitoa Real Madrid kwenye La Liga na anakusanya takwimu kuangalia kama kunauwezekana wakujiunga kwenye baadhi ya kubwa barani ulaya Ligi ambazo zilitajwa ni Ligi Kuu ya England EPL, Ligi ya Italia Serie A’, au Ligi ya Ujerumani Bundesliga. Sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na klabu hiyo kuwa na migongano na Rais wa La Ligi Javier Tebas.

Mapema Leo Los Blancos walitoa taarifa ya kukanusha taarifa hizo

“Kutokana na habari iliyochapishwa leo na gazeti la Mundo Deportivo, ambayo inasema kwamba klabu yetu ina uwezekano wa kuhama LaLiga kwenda Ligi Kuu England, Real Madrid inataka kusema kwamba habari hii ni ya uwongo kabisa, na ya kupuuzwa na isiyowezekana na imekusudia kuvuruga shughuli za kiutendaji za klabu.” Ilisema taarifa ya Real Madrid

Lakini pia kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Ligi Kuu England haitowezekana kwa Madrid kujiunga na Ligi hiyo kwani timu pekee zinazozoruhusiwa kucheza kwenye Ligi hiyo tajiri Duniani ni kutoka Wales pekee.