
Jamii ya wafugaji wa kabila la wamasai wanao ishi mpakani mwa wilaya ya Longido mkoani Arusha na wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro imedhamiria kutumia viongozi wa kimila kutoa elimu ya kupambana na ugojwa wa UKIMWI, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serikali kuakikisha wanapiga vita ukeketaji kwa watoto wa kike.
Hayo yamesemwa na na kiongozi wa kimila Benedict Olumolo wakati wa kumsimika kiongozi wa kimila, Legwanani Sembeta Msanga wa ukanda wa odimeti, amesema kuwa kwa sasa viongozi wa kimila wameelimika na wamefanikiwa kwa kiasi kupiga vita mila ambazo hazina faida kwa kwa jamii.
Amesema kwa sasa viongozi wa kimila, wana kazi ya kuhamasisha jamii kumpeleka mtoto wa kike shule badala ya kumuozesha kwa lengo la kupata pesa, ambapo wengi wa watoto wa kike hupoteza maisha kutokana na ndoa za utotoni na hasa kupata maambukizi ya ugojwa wa UKIMWI.
Paul laiza ni kiongozi wa kimila kwa rika kubwa la kabila la wamasai amesema amefanikiwa kupiga marufuku ngoma za usiku zinazo fahamika kama lesoto, ambapo vijana wa kabila hiyo huzitumia kama njia ya kujamiiana.
Akiongea mara baada ya kusimikwa kuwa Legwanani Sembeta Msanga amesema kuwa ana matumaini ya kuungwa mkono na jamii yote ya Tanzania ili aweze kufanikisha kwa kipindi chake hiki kupambana na mila potofu zinazo wakandamiza wanawake wa jamii hiyo ikiwemo ukeketaji hali inayo wasababishia kupata ugojwa wa UKIMWI.
Hata Hivyo amesema kuwa watafanikiwa kutokomeza mila hizo endapo mashirika mbalimbali yenye wataalamu Yataendelea kutoa elimu kwa jamii yao ya kabila la wamasai.