Wednesday , 26th Nov , 2014

Vilabu shiriki vya Ligi Tanzania Bara vimetakiwa vimetakiwa kuona umumihu wa kuhudhuria katika mashindano mbalimbali ya kukuza vipaji kwa vijana ili kuweza kupata vijana wenye vipaji ambao wataweza kunufaisha timu pamoja na taifa kwa ujumla.

Akizungumza jijini Dar es salaam,Mwenyekiti wa kamati ya Soka kwa vijana,Ayubu Nyenzi amesema bila kuwa na hulka kwa vilabu kuwa na muendelezo kwa vijana,soka la Tanzania litaendelea kuwa tegemezi kwa kuwa na vijana kutoka nje ya nchi ambao uwezo wao katika soka unalingana na wachezaji wa Tanzania.

Nyenzi amesema mashindano ya kuinua vipaji hunufaisha vilabu ambavyo huwa na wachezaji hao hadi siku za mbeleni na pia itasaidia kiuchumi kwani utasajili vijana ambao atakuwa faida ndani ya nch