Monday , 24th Nov , 2014

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda, Maurice Kirya ambaye pia ana kipaji kizuri cha uhudumu wa mgahawa, amejipanga kwa ajili ya kupamba sherehe ya Krismasi akishirikiana na kwaya kwa ajili ya siku hiyo kubwa.

msanii wa muziki wa Uganda Maurice Kirya

Kirya amesema kuwa, kwa sasa anatafuta timu ya kwaya ambayo watakuwa tayari kwa ajili ya kushirikiana naye katika mpango huu ambao utafanyika tarhe 4 mwezi ujao Jijini Kampala nchini Uganda.

Kirya kwa sasa anafanya vizuri na video mpya kwa ajili ya kuwapa moyo mashabiki wake, akiwa ameipatia jina Keep on Walking akishirikiana na Kwaya ya Africa Children kutoka Uganda.