Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

TFF yafafanua adhabu ya Mwakalebela

Tuesday , 6th Apr , 2021

Shirikisho la mpira wa miguu nchini 'TFF' limefafanua kuwa adhabu aliyopewa makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kuwa imeegemea kwenye uapnde wake wa uongozi wa klabu na si kwenye masuala mengine ya kama vile kumzuia asifuatilie taarifa za michezo.

Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini, Clifford Mario Ndimbo.

Akizungumza na EATV, Ndimbo amejibia malalamiko ya makamu mwenyekiti huyo aliyefungiwa kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 5 na faini ya shilingi milioni 7 kuwa, siku tatu zilizopita alisema amezuiwa asisome magazeti ya michezo wala kutazama luninga.

Ndimbo amesema “Kama ambavyo taarifa ya adhabu ulivyosema, na ni tofauti na alivyoielezea kwamba haruhusiwi hata kusoma magazeti au ikifika kwenye taarifa za michezo azime TV asiangalie. Adhabu aliyopewa ni kwamba majukumu yake ambayo amekuwa nayo ndipo aadhabu ilipoegemea”.

“Asijihusishe na majukumu hayo ya kiuongozi kwa muda huo ila mengine kuhusu kutokusoma magazeti labda alikuwa anafurahisha genge tu”.

(Aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela ambaye kwasa amefungiwa miaka 5.)

Ndimbo amesema Mwakalebela amefungiwa kimajukumu ya Uongozi lakini ana nafasi ya kushuhudia michezo viwanjani kama mashabiki wengine.

“Linapokuja suala la kwenda uwanjani hilo sio kujishugulisha na suala la uongozi wa mpira na maana  yake umekwenda kama mtazamaji mwingine”.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya