Wachezaji wa Simba SC na Namungo FC
Mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Yanga dhidi ya Azam majira ya saa 10:00 jioni na usiku majira ya saa 8:15 kutakuwa na nusu fainal ya pili inayohusu Simba dhidi ya Namungo. Washindi watakutana katika fainali Jumatano tarehe 13/1/2021.
Michuano hii iliyoanza 5/1/2021 ilishirikisha timu 9, tano kutoka bara ambazo ni Simba, Yanga, Namungo, Mtibwa na Azam, huku visiwani wakiwa na timu nne Jamuhuri, Chipukizi, Mlandege na Malindi, lakini katika hatua ya nusu fainali hizi, zimehusisha timu zote kutoka Tanzania Bara.
Kikosi cha Yanga SC na wachezaji baadhi wa Azam FC
Aliyekuwa bingwa mtetezi Mtibwa Sugar, ametolewa rasmi katika mashindano haya, baada ya kuruhusu kupoteza mchezo mmoja na kushinda moja hivyo kukosa tiketi ya 'mshindwa bora'.
Mashindano haya yaliyoanza mwaka 2007 yameshuhudia timu za Tanzania bara zikifanya vyema zaidi kwa kutwaa ubingwa mara 10 katika misimu 13 ya mashindanano, Azam mara 5 Simba 3 Yanga 1 na Mtibwa mara 1.