Thursday , 6th Nov , 2014

Yale maonesho makubwa ya mavazi na tuzo za ubunifu wa mavazi zitafanyika katika hoteli ya Sea Cliff kuanzia tarehe 5 hadi 7 disemba jijini Dar es Salaam.

Swahili fashion week mwaka huu itakusanya wabunifu 24 kutoka ndani na nje ya Tanzania watakaoonesha mitindo na ubunifu wao wenye kuendana na wakati utakaoshika soko la Afrika mashariki.

" Swahili Fashion week mwaka huu ina lengo la kuifikia jamii zaidi na kuendeleza vipaji katika tasnia ya mitindo na ubunifu wa mavazi. Lengo ni kuendeleza vipaji vya wabunifu wa ndani ili waweze kujulikana kimataifa zaidi". Amesema Washington Benbella meneja mradi wa Swahili fashion week.

Ikiwa ni mwaka wa 7 mwaka huu mashindano ya wabunifu chipukizi (EDC) yatajumuisha washiriki 9 ambao watatengeneza mavazi yao na mshindi atachaguliwa tarehe 5 Desemba wakati wa mashindano hayo. Maonesho haya pia yatajumuisha maonesho ya bidhaa zinazotengenezwa na wabunifu kwa siiku zote tatu (shopping festival). Swahili Fashion week itamalizika kwa tuzo maalum za mitindo zitakatolewa kwa watu mbalimbali.