Friday , 2nd Oct , 2020

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Wtu Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Taasisi ya Don Bosco Networks Tanzania imekamilisha awamu ya pili ya mafunzo stadi za kazi kwa vijana zaidi ya elfu tano nchini.

Baadhi ya wahitimu wakiwa katika sherehe za mahafali katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yalidhaminiwa na Serikali kwa lengo la kukuza ujuzi wa vijana, kukidhi soko la ajira pamoja na kuongeza wigo kwa vijana kujiajiri.

Akizungumza katika mahafali hayo Mkuu wa Chuo cha Don Bosco Osterbay Father Babu Augustin amesema kuwa kwa Dar es Salaam pekee vijana 1100 wamehitimu mafunzo hayo.

Kwa upande wao wahitimu wa mafunzo hayo wametoa wito kwa Serikali kuendeleza mradi huo kwani unasaidia vijana wengi.