Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.
Kamanda Mambosasa amesema kutokana uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo umewakamata na kuwa watachukuliwa hatua za kupelekwa Mahakamani na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria na na ametoa onyo kwa wale wote wanaondelea kufanya vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwaomba wananchi kutoa taarifa wanapobaini kuwepo kwa matukio kama hayo.
Amewataja watuhumiwa hao kutoka mataifa mbalimbali ya kigeni kwa tuhuma za kufanya uhalifu kwa njia mtandao (CYBER CRIME) na kuwataja Watuhumiwa hao kuwa ni ADEWALE NUREN OYEDES (34) Raia wa Nigeria ,IBRAHIM DARBEY (44) Raia wa Liberia CREAM MILTON ELIAS (38) Raia wa Liberia ,BASUBE DOMINIC (44), Raia wa DRC ,PRINCE TITO (46), Raia wa Liberia, SIBONGILE ARHUR (44), Raia wa Afrika Kusini. NA BALJIT SINGH (28), Raia wa India.
Aidha Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kujifanya maofisa usalama wa Taifa, Polisi na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao ni PATRICK TARIMO (32), Mkazi wa Mwenge, anajitambulisha kama afisa usalama wa Taifa. Na CASTORY WAMBURA (57), Mkazi wa Kibamba, anajitambulisha kama ofisa wa Polisi na kwamba watuhumiwa wote wawili wamekuwa wakitapeli raia wema kwa kujifanya waajiriwa wa Idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi.
“Mtuhumiwa Patrick Tarimo mnamo tarehe 10/08/2020 alijipatia kiasi cha Tsh 20,000,000/= kutoka kwa raia wa kigeni ambapo alimkamata na kujitambulisha kuwa yeye ni afisa usalama wa Taifa na kufanikiwa kujipatia kiasi hicho”alisema Mambosasa
“Kwa upande wa mtuhumiwa Castory Wambura mnamo tarehe 21/08/2020 alitapeli kiasi cha Tsh 15,000,000/= kutoka kwa wafanyabiashara watano wa kariakoo, ambapo alijitambulisha kuwa yeye ofisa wa Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)”