Friday , 4th Sep , 2020

Msanii wa singeli hapa nchini Manfongo amesema kuna muda alikuwa akipita mtaani kwao maeneo ya Tandale na Kijitonyama alikuwa anatembea na watu zaida ya 100 hadi 300.

Msanii wa singeli Manfongo

Manfongo ambaye kwa sasa amehamia Tabata amesema kitendo hicho kilikuwa kinatokana na upendo, sapoti anayoipata kutoka kwa mashabiki zake na watu wa mtaani kwao ambao wakimuona walikuwa wanamfuata nyuma.

"Ilikuwa inatokea kwa sababu ya watu walivyokuwa wananikubali, nilivyoondoka maeneo ya Tandale na Kijitonyama niliena kuishi Tabata, kwa hiyo nilivyokuwa naenda kuwatembelea na kuwasalimia mitaa yao nikipaki gari yangu tu  watu wananifuata mara nashangaa watu wamekuwa wengi kutokana na upendo na sapoti yao kwangu"

Aidha Manfongo ameongeza kusema watu hao walikuwa wanamfuata kwa ajili ya kuwazingatia kama kuwapa pesa kwa hiyo ndiyo maana ilikuwa kawaida kwake kutembea na kundi la watu wengi nyuma yake.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.