
Daniel Dubois
Dubois mwenye umri wa miaka 27 alilazimika kujiondoa katika kutetea mkanda wake wa IBF dhidi ya Joseph Parker wa New Zealand nchini Saudi Arabia siku ya Jumamosi kwa sababu ya ugonjwa lakini pambano dhidi ya Usyk mshindi wa mkanda wa WBO, WBA na WBC bado lipo
Dubois dhidi ya Usyk walipigana Agosti 2023 na Usky kufanikiwa kushinda kwa raundi 9 na baadaye Dubois akitangazwa kuwa bingwa wa IBF Juni 2024 baada ya Usyk kushindwa kuutetea mkanda huo
Kwa upande mwingine Usyk alipambana na Tyson Furry na kushinda mkanda WBO,WBC, WBA na kuwa bondia wa kwanza wa uzani wa juu kumiliki mikanda minne mikubwa katika uzani huo