Jumatatu , 24th Feb , 2025

Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa, wanajeshi wa Israel wamevamia katika maeneo tofauti ya mji wa Jenin katika Ukingo wa Magharibi alfajiri ya leo Jumatatu, katika maeneo ya magharibi mwa Jenin.

Kifaru cha kijeshi cha Israel kwenye Oparesheni Palestina

Haya yanajiri baada ya jeshi la Israel kuzidisha operesheni zake za kijeshi kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi siku ya Jumapili, kama sehemu ya kile walichokiita Operesheni ya "Iron Wall," ambapo magari ya kijeshi ya kivita yaliingia Ukingo wa Magharibi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 20.

Wanaharakati na waandishi wa habari walifuatilia kuingia kwa vifaru vinne vya Israel kutoka lango la Maqbila katika uwanda wa Marj Ibn Amer kuelekea mji wa Jenin na kambi yake, ambapo operesheni ya kijeshi ya Israel inaendelea kwa siku ya 34 mfululizo.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Israel, vikosi vya Israel vinafanya kazi ya kupanua wigo wa operesheni zao za mashambulizi katika eneo hilo kwa lengo la kuzuia mashambulio ya silaha nzito kutoka Brigedi ya Nahal na Kitengo cha Duvdevan kinashiriki katika operesheni katika vijiji vya eneo la Jenin lenye uhusiano na Brigedi ya Menashe, pamoja na juhudi za kijeshi za kijeshi zinazojumuisha kitengo cha kivita.