Jumatatu , 24th Feb , 2025

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Vatican imeeleza kuwa vipimo vya damu alivyofanyiwa Papa Francis vilionyesha kwamba alikuwa na changamoto ndogo ya awali ya tatizo la figo ambalo limeelezwa linaweza kudhibitiwa.

Papa Francis

Taarifa imeeleza kuwa hali ya Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 bado ni mbaya, lakini tangu usiku wa kuamkia jana Februari 23 hajapata zaidi matatizo ya awali ya upumuaji yaliyokuwa yakimsumbua, huku akiendelea na huduma 

Papa Francis ambaye amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki moja sasa jana alishiriki misa takatifu pamoja na wale ambao wamekuwa wakimuuguza katika chumba maalum alicholazwa katika hospitali ya Gemelli mjini Roma.