Eatv leo imepita katika mitaa ya Tandale jijini Dar es Salaam na kushuhudia vifaa vingi vya ujenzi vilivyotumika ambapo akizungumza mfanyabiashara Ally Mkule ambaye ni mfanyabiashara wa muda mrefu sokoni hapo amesema kwa sasa ile adha ya kusumbuliwa na askari viongozi wa Halimashauri haipo tena jambo linalowafanya kuendesha biashara hiyo kwa amani huku wakitengeneza faida kupitia biashara hiyo
Kwa upande wake Abdala Pazi amesema kuwa biashara hiyo kwa sasa imeshamiri katika maeneo mengi ya jiji amabzo zinahuisisha ununuzi wa bidhaa zilizokwishatumika na kusifu kutoa fursa za ajira kwa vijana wengi ambao wamejitenga na makundi ya uhalifu.
Aidha wafanyabiashara hao wa samani na vifaa vilivyotumika wamewataka wananchi kutokuwa na hofu kununua ama kuuza vifaa vilivyotumika kwani serikali imewapa nafasi pekee ya mauzo ya bidhaa hizo kulingana na ubora wake.