Monday , 13th Apr , 2015

Watu 18 wamekufa na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali ya basi la Nganga safari ajali hiyo iliyotokea leo katika kijiji cha msimba tarafa ya mikumi katika barabara ya Morogoro Iringa mkoani Morogoro nchini Tanzania.

Basi la Nganga linavyoonekana baada ya ajali hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Leonard Poul amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili asubuhi na chanzo chake ni Basi hilo la Nganga lenye kufanya safari zake Mbeya kwenda Morogoro kugongana na Lori aina ya Fuso katika eneo la Ruaha Iyove na kuongeza kuwa mwendo kasi wa dereva wa basi hilo kutaka kulipita Lori hilo pasipo kuwa na tahadhari ndiko kulipeleka ajali hiyo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa madereva wote wamefariki dunia na kuwa majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito katika mkoa wa Morogoro.

Kwa upande wake Mganga wa Hospitali ya Mtakatifu Kizito Dkt. Bonivanture Buyagabuyaga alithibitisha kupokea miili ya marehemu 18 ambayo ilikua imeteketea kwa moto.