Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Humphrey Polepole
Akizungumza hilo kupitia kipindi cha Supa Breakfast ya East Africa Radio wakati yupo kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Humphrey Polepole amesema,
"Nilisema kuna kazi kama mbili na nusu, kwanza ni kumchagua mgombea wa CCM, pili ni kumtambulisha mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano, tatu ni kumtambulisha mgombea wa Urais wa Zanzibar, ushindi wa mwaka huu ni vizuri kuwaambia watu mapema na kuwaanda kisaikolojia, kwa sababu tumefanya utafiti wa Tanzania mwezi wa pili, ushindi wa mgombea Urais CCM ni asilimia 90, hiyo ilikuwa kabla ya Corona kuingia".
Pia Humphrey Polepole amesema kazi ya CCM ndani ya chama ni rahisi kwa sababu hawafanyi kazi kwa matakwa ya mtu kama vyama vingine, na kila wanachokifanya kimeandikwa kwenye katiba.



