
Balozi Ali Abeid Karume akichukua fomu
Balozi Ali Abeid Karume ambaye pia ni mtoto wa muasisi wa Taifa hilo, hivi sasa ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar katika Serikali ya awamu ya Saba chini ya Rais Dkt. Ali Mohamed Shein.
Ali Karume anakuwa mtu wa Pili kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar ambapo Mbwana Bakari Juma alikuwa wa kwanza kufika ofisini hapo na kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.
Mara baada ya kuchukua Fomu Balozi Ali Abeid Karume amesema kwamba iwapo chama cha Mapinduzi CCM kitampa ridhaa ya kuwa mgombea wa nafasi hiyo na kuwa Rais wa Zanzibar, anatarajia kuendelea dhamira ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuyalinda, kulinda Muungano wa Tanganiyika na Zanzibar na kuendeleza Sera za CCM.
Pia Balozi Karume amesema, "nitapenda ugawaji wa Ardhi uendelee hasa kwa wananchi ambao wanaihitaji kwa masuala ya Kilimo, Ujenzi pia tutajenga makazi bora".