Wednesday , 10th Jun , 2020

Jumla ya wabunge 69 wa CHADEMA wakiwemo waliohama chama hicho, wameitwa na TAKUKURU makao makuu kwaajili ya kuhojiwa kuhusiana na matumizi ya fedha ambazo walikuwa wakikatwa wabunge wote, ambapo hivi karibuni matumizi ya fedha hizo yalilalamikiwa na baadhi ya wabunge.

Afisa uhusiano wa TAKUKURU Doreen Kapwani

Taarifa ya TAKUKURU iliyotolewa na Afisa uhusiano Doreen Kapwani, imeeleza kuwa, fedha hizo ni zile ambazo zimelalamikiwa na wabunge waliokihama chama hicho.

Aidha TAKUKURU wameeleza kuwa tayari wameshawahoji viongozi wa CHADEMA, viongozi waliowahi kuwa CHADEMA, Wabunge waliotoa taarifa, Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wengine.

Tazama Video hapo chini akieleza zaidi.