
Msanii Barakah The Prince na Najdattani
Najdattani amesema hivyo baada ya kuwepo na taarifa juu ya kutajwa kwa mpenzi wake huyo, kwamba ndiye msanii anayeongoza kuwajibu mbovu mashabiki mitandaoni.
Akizungumza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital Najdattani amesema "Kiukweli amelifanyia kazi hilo jambo, sidhani kama kipindi cha hapa karibuni amemjibu mtu vibaya kuna muda inatokea kama binadamu, kuna comments zinakukwaza sana hadi ukapoteza muelekeo, huyu sio Barakah yule ambaye mmemzoea kwamba kila kitu kinamkasirisha ndiyo maana amejitafuta kwenye hiyo miaka miwili".