Sunday , 3rd May , 2020

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema anafikiria siku zijazo huenda akaruhusu kurejea kwa Ligi Kuu soka Tanzania Bara na michezo mingine kwa kile alichokisema ili kuwapa nafasi wananchi kutazama michezo hiyo, kwenye TV.

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mwakyembe

Rais Magufuli amesema hayo wakati akimuapisha Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba mkoani Geta, ambapo amesema hakuna mwanamichezo ambaye amepata madhara makubwa juu ya ugonjwa huo.

Rais Magufuli amesema kuwa "Siku za mbeleni ninafikiria kuruhusu Ligi ziendelee, ili watu wacheze wawe wanaangala kwenye TV na tuweke utaratibu mzuri, hata waliokuwa affected na Corona sijaona Mwanamichezo yeyote ambaye amedhurika sana kwenye hili"

"Siku za mbeleni ninafikiria kuruhusu Ligi ziendelee, ili watu wacheze wawe wanaangala kwenye TV na tuweke utaratibu mzuri, hata waliokuwa affected na Corona sijaona Mwanamichezo yeyote ambaye amedhurika sana kwenye hili" - Rais @MagufuliJP #JPMKumuapishaMwigulu pic.twitter.com/mH3zdG1Oxw