
Kituo cha mafuta
EWURA imesema kuwa bei za mafuta zinazotangazwa kupungua hivi karibuni ni za mafuta ghafi (crude oil) nchini Marekani na siyo mafuta yaliyosafishwa (refined petroleum products). Punguzo hilo linatokana na kukosa mahali pa kuhifadhi mafuta hayo.
Tanzania haina mitambo ya kusafisha mafuta (refineries), hivyo mafuta yanayoingizwa nchini ni yale yaliyosafishwa tu. Pia hakuna Hifadhi ya Taifa ya kuhifadhi kwa wingi.
Hata hivyo, ikiwa mafuta yatashuka katika Soko la Dunia (Uarabuni) itachukua kipindi cha miezi miwili ndipo watanzania waone faida yake.
Taarifa kamili hii hapa chini.